April 23, 2018






DORTMUND, Ujerumani
MSHAMBULIAJI Jadon Sancho ameweka rekodi ya kuwa Muingereza mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao katika Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’.

Jadon aliweka rekodi hiyo juzi wakati alipoifungia timu yake ya Borussia Dortmund bao kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bayer Leverkusen. Ligi hiyo, hapa Bongo unaitazama kwa bei nafuu sana kupitia King’amuzi cha StarTimes.

Sancho alitupia bao hilo katika dakika ya 13 kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park, kutokana na mpira wa kona.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 pia alitengeneza asisti mbili kwa Maximilian Philipp na Marco Reus katika kipindi cha pili na hivyo kumfanya kuwa na siku nzuri.


Akizungumza mara baada ya mchezo huo, chipukizi huyo anasema: "Nilipata nafasi mara ya kwanza sikuitumia vizuri, ilinisikitisha kwa kuwa muda huyo matokeo yalikuwa 0-0.

"Nilipopata nafasi nyingine nikaitumia vizuri, nina furaha nimefunga bao langu la kwanza nikiwa hapa. 

"Limekuwa jambo gumu kurejea kwenye kikosi, kuwa fiti na sasa ninajisikia vizuri."


Sancho amekuwa Muingereza wa pili kufunga bao msimu huu katika Bundesliga, mwingine alikuwa ni Ademola Lookman wa RB Leipzig.

Chipukizi huyo alijiunga na Dortmund mwanzoni mwa msimu huu akitokea Manchester City, alicheza mchezo huo ukiwa ni wa tisa kwake na wa nne kuanza katika kikosi cha kwanza.




Neuer arejea uwanjani, kocha afunguka

MUNICH, Ujerumani
KOCHA Mkuu wa Bayern Munich, Jupp Heynckes amezungumzia juu ya kipa wake, Manuel Neuer ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita sasa kuwa ana mpango wa kumtumia kabla ya msimu huu haujafikia tamati.

Neuer, alikuwa majeruhi tangu alipoumia mguu katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mainz katika mechi ya Septemba 16, 2017, ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza tangu Ijumaa iliyopita.

"Tunafurahia jinsi anavyoendelea,” alisema Heynckes na kuendelea: 



"Tunafanya kila kitu kiwe sawa kwa sasa lakini ni mapema sana kuzungumzia kuhusu lini atarejea uwanjani, najua ninachokifanya, nina mpango naye muhimu.”

Bayern bado inasubiri kucheza fainali ya DFB Cup, pia ina mechi za Ligi ya Mabingwa pamoja na mechi chache za Bundesliga licha ya kuwa wameshatwaa ubingwa.

Kabla ya kuumia, Neuer alikuwa mmoja wa makipa bora duniani, kurejea kwake kunaweza kuwapa nguvu Ujerumani kuelekea katika michuano ya Kombe la Dunia ambayo pia itarushwa na StarTimes.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic