April 23, 2018





NA SALEH ALLY
BAADA ya matokeo ya sare ya bao 1-1 kati ya Simba dhidi ya wenyeji wake Lipuli FC ya Iringa kumeibuka mambo mengi sana ya ajabu. 

Kwanza niliona zile vurugu ambazo zilitokea na mashabiki wa Simba na Lipuli FC kurushiana maneno na baadaye ikawa ni kuchapana.

Mashabiki wa Simba baadaye walilalamika kwamba kulikuwa na kampeni ya kimkoa kwamba walipigwa kwa makusudi na askari polisi ambao walikuwa kila wakiona mwenye jezi ya Simba wanampiga.

Walilalamika kwamba ilionekana ni kampeni ya kimkoa kuhakikisha Simba wanapigwa na kunyimwa raha.

Lakini nilizungumza na mtu mwingine kutoka Iringa ambaye naye aliwalalamikia mashabiki wa Simba kwamba walionyesha dharau kwa askari kwa kuwa tu wanatokea Dar es Salaam.

Vitendo vya namna hii vinaashiria mambo mawili, suala la kutokuwa na upendo wa kimpira kwa upande mmoja kujikweza na kujiona ni bora zaidi au upande mwingine kuchukizwa na ukubwa wa upande mwingine, hivyo kupanga wanawakomoa.

Kama kila upande ungefika kwenye Uwanja wa Samora kwa lengo la kuangalia mpira na kuisaidia timu yao kufanikiwa, suala la vurugu lingekuwa ni nadra kabisa kutokea.

Pia inachangiwa na upande mmoja wa mashabiki pia kwenda na matokeo mfukoni hata kabla haujachezwa, jambo ambalo si sahihi hata kidogo.

Kwenda na matokeo lazima tutashinda kwa kuwa timu yetu inashinda kila siku ni kujivuruga. Kama itatokea matokeo yakawa si yale uliamini ndiyo mnaweza kuyapata, basi mwisho wake ni vurugu kama hizo.

Kuna haja ya kuheshimu misingi ya mpira na kuamini ili matokeo yapatikane, mpira huwa ni lazima uchezwe kwanza.

Mpira lazima uchezwe ili kujua nani kashinda au sare kwa wote. Badala ya kuamini au kuhesabu mabao yaliyofungwa hata kabla ya mpira kuchezwa na baadaye kutupiwa wavuni ili kuhesabu mabao.

Nilisikia jambo jingine ambalo kwangu naliona ni la watu wanaokosa weledi, wanaoenda na ushabiki njaa, ushabiki wa kutojitambua na ikiwezekana kutaka kuonekana wanaipenda Simba kama ambavyo imekuwa mashabiki wengi wakifanya hivyo kutaka kujionyesha kwa wengine badala ya kujali kuonekana kwa watu

Nilipita sehemu nikaukuta ule mjadala wa kwamba baadhi ya mashabiki wa Simba wamekuwa wakishangazwa sana na Selemani Matola kushindwa kuiunga mkono Simba.

Matola ni Kocha Mkuu wa Lipuli FC kikazi, lakini kwa kufuata vyeti yeye ni msaidizi wa Amri Saidi ambaye pia alikuwa beki wa kati wa Simba.

Hivyo, mashabiki hao ninaopenda kuwaita ni njaa, waliona sahihi Matola kuiunga mkono Simba huenda kwa kuwashawishi wachezaji wake kuiachia Simba ishinde, jambo ambalo ni upuuzi wa hali ya juu kwa kiwango cha lami.

Waliokuwa wanajadili walionekana kumshangaa Matola kwa kutoisaidia Simba. Huku wakiwataja makocha wengine wa timu za Ligi Kuu Bara kwamba wamekuwa wakiisaidia Yanga.

Kwanza hawakuwa na uhakika na hilo, jambo ambalo ni upuuzi mkubwa. Kama limewahi kutokea, pia ni upuuzi wa hali ya juu na lazima wajue timu bora ni ile inayoshinda bila ya matokeo ya kupanga.

Matola ni kocha wa Lipuli, anapaswa kuisaidia Lipuli na si Simba ambayo anatakiwa kuifunga. Achana na hiyo, waliokuwa wanasema hivyo wanaonyesha upeo wao katika mchezo wa soka ni hovyo na wabaishaji wakubwa.

Soka hili limeingiwa na mashabiki wa hovyo ambao wanahisi wanajua kila kitu hata kama wameanza kushabikia hizo timu hasa Yanga na Simba, miaka mitatu minne iliyopita.

Wababaishaji hawa ndiyo hupotosha mengi kwa kuwa wako wanaoaminiwa na kufanya mambo yaonekane tofauti. 

3 COMMENTS:

  1. Mr EDITOR,what I used to know and am still knowng is this,you must hide IDENTITY,sasa vip wewe unajiweka uchi?jaribu kuficha uyanga pale unapokua kwenye suala la kazi yako.

    ReplyDelete
  2. Always your a good editor mashabiki wa Simba wanakuona wewe yanga na wa Yanga hivo hivo wanakuona wewe ni Simba its so funny yani...Wanakufanya kazi yako imekua nyepesi mno

    ReplyDelete
  3. Keya Said unajisumbua bure ndugu yangu. Mwandishi anaye comment stori za vijiwe vya kahawa hafai kutiliwa maanani.Aliweka stori ya mchezaji kukosa mechi kwa sababu ya yellow card.Ameitoa bila sababu za maana. Kama ilikuwa ni stori ta vijiwe vya kahawa unamchukulia serious vipi?Hawezi kuwa objective hata mara moja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic