April 30, 2018



Na George Mganga

Afisa Habari wa zamani wa klabu ya Yanga, Jerry Muro, ameipongeza Simba kwa ushindi ilioupata dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu bara uliopigwa Jumapili ya Aprili 29 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Erasto Nyoni kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Shiza Kichuya katika dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza.

Muro amewapongeza Simba huku akimsifu Ofisa Habari wa timu hiyo, Haji Manara kwa kuwahamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanjani ili kuipa timu yao hamasa.

Mbali na hayo, Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Muro amewapa pole Wanayanga wote kwa ujumla huku akiwaomba waige mfano kwa Simba namna walivyojitoa kuhamasisha mashabiki wao kujitokeza kwa wingi uwanjani.




Muro ameeleza hayo akiamini kuwa shabiki ni mchezaji namba 12 hivyo anapokuwepo Uwanjani hutoa motisha nzuri kwa wachezaji ili wapate morali ya kujituma.


3 COMMENTS:

  1. @Jerry Muro ni kweli hamasa ni muhimu sana,nadhani hili ulishaliona mapema nadhani wewe kama mkereketwa wa kutupwa wa yanga ulipaswa kulifanyia kazi kabla maji hayajatumwagikia kwa kutumia taaluma yako hatakama haupo ktk uongozi,pengine matokeo yangekuwa tofauti,Sio@mtu kajaliwa kywa na kipaji cha kuhamasisha,wito wangu kwsko tumia kipaji chako /taaluma yako kuitoa yanga ilipo,washabi/wapenzi wataelewa tu,Yanga ya watanzania ,daima mbele.

    ReplyDelete
  2. Muro fair play ni muhimu sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic