Na George Mganga
Mapema baada ya mchezo kumalizika, mashabiki hao walianza kutupia lawama kwa Nsanjigwa, wakidai kuwa hana mbinu za kuendelea kuisaidia timu hiyo ipate matokeo, na badala yake ameisabishia kupoteza mchezo.
Kwa mujibu wa Spots Xtra ya Clouds FM, mashabiki hao waliokuwa wamepandisha hasira kutokana na kufungwa na watani zao wa jadi Simba, wameuomba uongozi wa Yanga kuachana na Nsanjigwa wakieleza kuwa hana ujuzi wa kuendelea kuinoa Yanga.
Yanga ilikubali kufungwa bao moja na Simba katika mchezo huo uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, bao hilo likitiwa kimiani na Erasto Nyoni kwenye dakika ya 37.
Kwani Nsajigwa alicheza uwanjani?
ReplyDeleteNamfahamu vzr Nsajigwa nilishasemaga hafai kuwa kwny bench la ufundi la Yanga, kwanza itikadi yake mnyama tangu anacheza fullback Yanga
ReplyDeleteHawa walitaka ushindi ambao hawastahiki kuupata mbele ya mnyama na kwa miaka ya karibu msitegemee. Hau mliokuwa mnawategemea, kwa jana hawakuwa na jipya ila kutemea watu kamasi chafu zenye kutoa uvundo. Bado watema makoo watakusaidieni nini. Hao wote waliihama Simba na matusi juu na hebu zitazameni hali zao walivo. Ndio mtaowategemea huko Al Jeria. Hebu wajaribu huko kutemea makohoo kama hawatarejea vibogoyo
ReplyDelete