Kocha Mkuu wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesema kama Simba itafanikiwa kushinda mechi zake mbili zijazo ikiwemo ya Yanga basi itakuwa imeshatwaa ubingwa wa msimu huu kutokana na kasi waliyonayo.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 55, nyuma ya Yanga inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 47. Azam kabla ya mechi ya jana ilikuwa na pointi 45 katika nafasi ya tatu.
Tayari Simba imebakiza mechi saba ambazo sawa na pointi 21 wakati Yanga ikiwa ina mechi nane sawa 24.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Julio alisema: “Unajua kila kitu mipango, Simba sasa hivi ni wakati wao, wapo vizuri na wanastahili kuendelea kushinda kwa sababu kikosi chao kipo vizuri, kama wakiendelea na kasi hii kwa kushinda mechi mbili zijazo ikiwemo ya Yanga basi watakuwa mabingwa na hilo halina mjadala.
“Nadhani Yanga kwa sasa ingeachana na suala la ubingwa na kuendelea kuijenga timu yao kwa sababu imenifurahisha falsafa yao kutoa nafasi kwa vijana ambao naamini watakuja kuwa tishio katika msimu ujao kama ilivyofanya Simba miaka iliopita".
CHANZO: CHAMPIONI
Hapo Julio umesema lakini sio kuifundisha timu hiyo ambayo kwa sasa inaelekea kusikojulikana
ReplyDeleteMtu km Julio apewe yanga BC makocha wameisha
ReplyDelete