Baada ya kutokuwa na mwenendo mzuri na kikosi cha Mbao FC msimu huu, inaelezwa kuwa Kocha Ettiene Ndayiragije, ameikacha timu na kutimkia kwao Burundi.
Kocha huyo hakuonekana katika benchi la ufundi jana dhidi ya Majimaji FC huku Msaidizi, Flugence Novatus akisimamia kuiongoza timu katika mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Mara ya mwisho Ndayiragije kuiongoza Mbao FC ilikuwa ni dhidi ya Lipuli FC iliyomalizika kwa matokeo ya 0-0 huku mashabiki wakimuandama aiachie timu ambapo baada ya mtanange huo kumalizika alipewa ulinzi na askari.
Taarifa zilizo chini ya kapeti kutoka Mbao zinaeleza kuwa tayari Kocha huyo ameshaondoka huku Novatus akikaimu nafasi kwa muda.
Mbao ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi msimu huu kwa kujikusanyia pointi 24 ikiwa imecheza mechi 25.
Hivi karibuni, mashabiki walivamia uwanja baada ya mechi wakidai kocha huyo alipanga wachezaji kadhaa akiacha walio muhimu nje.
Kuna tatizo makocha wa kigeni wanaanza kuondoka mmoja badala ya mwengine. Kule Dodoma Fc Julio kaondoka bila ya kuaga:) Lwandamina Yanga inasemekana alivaa baibui kujiziba uso wake pale aiport asijulikane matokeo yake tumekuja mshuhudia akimega bia yake jukwaani kule Zambia akiangalia mechi yaani sirahisi kuamini kama lwandamina hakuwa na taaluma ya kusafiri na ungo wa kichawi? Huyu Mrundi nae inasemekana alijichanganya na kundi la wakimbizi wanaorudi kwao ili asijulikane. Julio wakati serikali ipo katika mikakati mizito ya kulihamishia jiji Dodoma yeye anarudi Daresalam kuna tatizo! Makocha wanatakiwa kuwa wastahamilivu wanatakiwa kujifunza kutoka kwa Wenger wa Arsenal. Kali Ongala nae Zamani tu kaibwaga maji maji kuna tatizo! Vyama mpira nchi nyingi duniani ni vitajiri kiasi kwamba vinauwezo wa kuvisaidia vilabu kujimudu sio tu kuwa na uwezo wa uhakika wa kulipa mishahara ya makocha na wachezaji lakini hata katika kuhakikisha kuwa vinamiliki miundo mbinu yao wenyewe kama viwanja vyao binafsi na miradi mbali mbali .
ReplyDeleteVyama vyetu vingi vya
Mpira huku kwetu Africa vinakosa utajiri wa Maarifa na ubunifu wa kiutendaji. Masuala ya hati miliki ya timu kama jazi na vifaa vingine pamoja na maenyesho ya mechi sio vita ya timu husika peke yake bali ni ya kitaifa. Uhamasishaji kwa wapenzi na wanachama kuwa wazamendo kwa timu zao kwa kuzisapaoti kwa hali na mali sio kazi ya klabu peke yake bali ni jukumu la vyama vyetu vya mpira pia, vya kitaifa na ngazi za wilaya. Lakini vyama vyetu vingi vya mpira Africa ni vyama vyenye kusubiri mgao wao kutoka kwa vilabu amabavyo vyenyewe vinashindwa kujimudu aidha kutokuwa na uwezo wa kujiendesha kutokana na kuwa na viongozi wa hovyo au uwezo mdogo wa kiuchumi. Nchi zetu ni nchi zinazoendelea kujijenga kwa hivyo kila taasisi inahitaji usimamizi wa karibu zaidi wakati wote tofauti na nchi zilizokwisha jengeka ambapo taasisi zake nyingi tayari zinamisingi inayoweza kujiendesha wenyewe na watu kuwa kama wasimamizi tu. Watanzania tupo walaini sana kukubali kushindwa takribani katika kila nyanja si michezo si maendeleo yetu wenyewe binafsi. Kwa mfano sioni sababu ya nchi yetu kupeleka washiriki katika mashindano kama ya Olympic au haya mashindano ya jumuiya ya madola. Tunapeleka washiriki kwenda kufanya nini? Tunatakiwa kupeleka washindani lakini washindani hatuna kwa nini tupeleke washiriki wanaokwenda kulipaka matope taifa miaka nenda miaka rudi?lakini tunarudi nyuma pale pale vyama vyetu vya michezo na taasisi husika ndiko kunako uozo wote huu na sio kwa wanamichezo. Kuna tatizo na wakati wa kulitatua ndio huu. Kazi ya kutumbua majipu bado kabisa kuna yale yaliojificha na mengine yamepakwa mafuta kiasi cha kuonekana hayana madhara lakini ukweli ni kwamba kuna baadhi ya taasisi hali ni tete sana hasa sekta ya michezo.
Na Julio anapiga hodi kwa yanga kutaka kuiongoza timu hio akijieleza ana uwezo kamili baada ya kuikimbia Dodoma
ReplyDelete