April 2, 2018





Milan, Italia
LEORNARDO Bonucci, juzi alikuwa mwanaume wa shoka tena alipofanikiwa kuifungia AC Milan lakini ikapata kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Juventus.

Hii ni picha halisi kuwa Juventus kwa sasa wanaweza kuwa kwenye picha halisi kuwa wanaukaribia kwa nguvu kubwa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’.

Mashabiki wa Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga) ambao wanatazama ligi hiyo kupitia King’amuzi kwa StarTimes, walimshuhudia staa wa Juventus, Paulo Dybala, akiifungia timu yake bao la kwanza katika dakika ya nane tu ya mchezo huo.

Staa wa Juventus aliyekuwa mgonjwa kwa muda mrefu kidogo, Juan Cuadrado, aliingia kwenye mchezo huo na kufanikiwa kuifungia timu yake bao la pili huku Sami Khedira akifunga la tatu.

Ushindi huu umewafanya Juventus kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi nne, huku Napoli ambao walikuwa wanapambana kwa nguvu kubwa kutwaa ubingwa huo msimu huu wakilala kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Sassuolo.

Awali, Sassuola walikuwa hawapewi nafasi kubwa ya kuwazuia Napoli kwa kuwa ni moja kati ya timu vibonde zaidi kwenye ligi hiyo.

Beki wa zamani wa Juventus, Bonucci, 30, ambaye aliondoka kwenye timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu, alipokelewa vizuri kwenye mchezo huo kutokana na kushangiliwa kwa nguvu kubwa kwenye Dimba la Allianz.

Hata hivyo, bao la beki huyo lilishangiliwa kwa nguvu kubwa na mashabiki wa timu pinzani kuonyesha kuwa bado wanamjali.

"Nimefurahia kwa kuwa Bonucci amefunga bao lakini nina furaha kwa kuwa Juventus wamepata ushindi,” alisema kocha wa Juventus.

"Lilikuwa jambo zuri sana kuendelea kupata ushindi, kuhusu Milan ni timu nzuri ambayo ina wachezaji wengi sana mahiri,” alimalizia kocha huyo.

Hiki kilikuwa kichapo cha kwanza kwa Kocha Gennaro Gattuso, kwenye Ligi Kuu ya Italia kwa mwaka 2018, akiwa alikuwa amefanikiwa kumaliza ubabe wake wa kushinda mechi kumi mfululizo kwenye ligi hiyo.

Kwa sasa Juventus wamefanikiwa kufikisha pointi 78 baada ya kucheza michezo 30 huku Napoli wakiwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 74. AC Milan kwa sasa wapo nafasi ya sita kwenye Ligi Kuu ya Italia.

“Lazima tuendelee kupambana, lazima tuendelee kuonyesha umwamba wetu kwenye ulimwengu huu wa soka, bila kupambana hakuna jambo lolote ambalo tunaweza kulipata, tutabaki na heshima kuwa tulikuwa na msimu mzuri lakini hatuna mafanikio yoyote,” alisema Gatusso baada ya mchezo huo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic