April 30, 2018



Na George Mganga

Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Shiza Kichuya, amezungumzia kitendo cha beki wa Yanga, kelvin Yondani kumtemea mate mchezaji wa Simba Asante Kwasi akieleza kuwa ni cha kukemewa.

Kichuya ameandika ujumbe mfupi kupitia Instagram unaoonesha kuchukizwa na kitendo hicho alichokifaya Yondani jana katika mchezo wa ligi ambao Simba walishinda kwa bao 1-0.

Kichuya ameandika kuwa tabia hiyo kwa wacheza haipendezi na ni ya kishamba hivyo inapaswa isiendelee kufanyika kwasbabu kuna maisha baada ya mpira.

"Mpira siyo vita, kumtemea mwenziyo mate ni kukosa ustaarabu na utu, tukemee hii tabia na tuache ushamba, kuna maisha baada ya mpira" ameandika Kichuya.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic