Ruvu ilikubali kichapo cha mabao 3-1 ikiwa ugenini huko Majimaji Stadium na kuifanya timu hiyo ipande juu kwa nafasi mbili mpaka ya 14 kwenye msimamo wa ligi.
Kifaru ameeleza kuwa amesikitishwa na matokeo hayo kutokana na rafiki yake Bwire kupokea kiasi hicho cha mabao hayo jana.
Msemaji huyo amempa pole Bwire akieleza kuwa jana ameshindwa kuwapapasa Majimaji na badala yake amepapaswa mwenyewe.
Aidha, Kifaru naye alishindwa kutamba nyumbani mbele ya Azam jana kufuatia kukubali kichapo cha bao 1-0 mjini Turiani, Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment