LICHA YA KUPIGWA 3-1, MASAU ASEMA MAJIMAJI HAINA UWEZO
Baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Majimaji FC, uongozi wa Ruvu Shooting kupitia Msemaji wake, Masau Bwire, umesema kuwa hauna uwezo wa kuwapapasa bali ni bahati tu imeangukia kwao.
Majimaji jana ilifanikiwa kuicharaza Ruvu kwa mabao hayo matatu katika mchezo wa ligi kuu bara uliopigwa mjini Songea.
Bwire amesema kuwa Majimaji ni ya kawaida licha ya kushinda hizo bao tatu huku akieleza kuwa haina uwezo wa kupapasa.
Msemaji huyo amekuwa akitamba kabla ya kucheza na wapinzani wake, kuwa lazima waipapase timu watakayokutana nayo lakini janakibao kimegeuka na wakapapaswa wao.
0 COMMENTS:
Post a Comment