April 29, 2018



Kikosi cha Azam FC jana kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Ushindi huo wa Azam umeiondoa Yanga kwa muda katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi na kuishushusa mpaka namba tatu.

Azam jana imefanikiwa kujikusanyia alama tatu muhimu na kufikisha pointi 49 dhidi ya Yanga walio nyuma kwa michezo mitatu dhidi yao wakiwa na pointi na 48.

Inawezekana Azam ikawa imekalia nafasi hiyo kwa muda kwasababu leo inacheza dhidi ya Simba, endapo itashinda itarejea tena kwenye nafasi hiyo ya pili.

Yanga inaingia kibaruani jioni ya leo ikiwa mgeni dhidi ya Simba, mchezo utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic