April 2, 2018



Kikosi cha Simba kimeanza safari asubuhi hii kuelekea Njombe tayari kwa mchezo wake wa kesho dhidi ya Njombe Mji FC.

Kikosi hicho kiliweka kambi ya muda mfupi mkoani Iringa ambapo jana kilifanya mazoezi katika Uwanja wa Samora mkoani humo.

Simba itakuwa ina kibarua cha mechi ya ligi dhidi ya Njombe Mji FC itakayopigwa kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini humo.
 

1 COMMENTS:

  1. Njombe mji haitakuwa mteremko hata kidogo kwa Simba. Wachezaji wa Simba wajiandae na sapraiz kutoka kwa wachezaji wa njombe. Njombe wapo kwao,wapo kwenye ukingo wa kutumbukia darajani na zaidi ni hamasa binafsi kwa wachezaji wa Njombe mji kuonesha vipaji vyao ili kuwavutia viongozi wa Simba na wanahaki ya kufanya hivyo kwani licha ya maslahi Simba ni miongoni mwa vilabu vyenye huduma bora ya makocha na ushindani wa namba kwa mchezaji mwenye kutafuta mapinduzi ya kiwango chake kwa wale wenye malengo ya kufuata nyayo za kina Samata na msuva. Kwa upande wa Simba mechi hiyo si ya kupoteza naweza kusema ni muhimu zaidi ya mechi ya Almasry. Tungependelea kuona Simba ikirudi kimataifa mwakani kwani licha kutolewa mapema mwaka huu lakini kwa kweli wametujaza matumaini yakwamba wanauwezo wa kutuwakilisha kiheshima na tunaimani mwakani wanaouwezo wa kufanya vizuri zaidi. Kila la kheri kwa timu zote mbili.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic