NIYONZIMA KUPAA USIKU HUU KUELEKEA RWANDA
Kiungo wa klabu ya Simba, Haruna Niyonzima, anatarajia kuondoka usiku huu kuelea Kigali, Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria msiba wa dada yake aliyefariki leo.
Niyonzima amefiwa na dada yake anayefahamika kwa jina la Sumaya Twizemana ambaye anamfuata baada ya yeye kuzaliwa.
Niyonzima amekuwa hana msimu mzuri na Simba kufuatia kushindwa kuitumikia klabu yake kwa muda mrefu sababu ya kuandamwa na majeraha.
Nyota huyo wa Simba hatoweza kucheza mechi dhidi ya Yanga kutokana na ushiriki wake katika msiba wa dada yake na haijajulikana atarejea baada ya muda upi.
Blog ya Saleh Jembe inamtakia pole za dhati Niyonzima, kutokana na wakati mgumu alionao hivi sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment