Kocha mpya wa Yanga, Mwinyi Zahera leo ametua katika makao makuu ya klabu hiyo na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa yanga, Charles Boniface Mkwasa.
Zahera amefanya mazungumzo ya muda wa takribani saa moja na Mkwasa kabla ya kutembezwa sehemu kadhaa katika ofisi za klabu hiyo.
Kocha huyo, anachukua nafasi ya George Lwandamina ambaye ameondoka Yanga na kujiunga na Zesco ya kwao Zambia.
Zahera alitua usiku tayari kumalizana na Yanga na mambo yakiwa safi ataondoka zake kwenda Morogoro ambako Yanga imepiga kambi.








Nimtakie kazi nzuri zahera ya kuendeleza pale alipoacha lwandamila
ReplyDelete