April 7, 2018




Na George Mganga

Kikosi cha Majimaji kinashuka dimbani jioni ya leo kikiwa ugenini dhidi ya Mwadui FC huko Shinyanga.

Majimaji imekuwa na msimu mbaya ambapo mpaka sasa ipo mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 16 pekee.

Mwadui FC itakuwa inaikaribisha Majimaji ikiwa kwenye nafasi ya 13 katika msimamo na ikiwa ina pointi 20.

Endapo Majimaji itapata matokeo, itakuwa imejinasua mkiani mwa ligi kwa kufikisha pointi 19 na kuishusha chini Njombe Mji Fc iliyo na alama 18.

Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni ya leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic