April 26, 2018



Kocha Pierre Lechantre hakutaka kikosi chake kifanya mazoezi mbele ya mashabiki.

Mfaransa huyo aliamuru mageti ya Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kufungwa ili aendelee na kazi yake kwa uhakika zaidi.

Uamuzi huo ulipitishwa leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na mashabiki waliotaka kuangalia wakajikuta wanalazimika “kupiga chabo”.

Mashabiki wengi walikuwa milangoni wakitumia upenyo mdogo kuishuhudia Simba ikifanya mazoezi ya mwisho.

Simba iko kambini ikijiandaa kuivaa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic