April 21, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Simba kimeshindwa kupata alama tatu na badala yake kimepoteza pointi mbili katika Uwanja wa Samora mjini Iringa dhidi ya Lipuli, mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo ulioanza kwa kasi zaidi kwa wenyeji wakionesha kuumiliki mpira zaidi ya Simba, walikuwa wa kwanza kujiandikia bao mnamo dakika ya 31 ya kipindi cha kwanza kupitia Adam Salamba.

Bao lilidumu kipindi cha kwanza ambapo mpaka Mwamuzi anapuliza kipyenga kwenda mapumziko, Lipuli walikuwa mbele kwa bao moja.

Kipindi cha pili Simba walijitahidi kuamka na kuanza kujibu mapigo baada ya Kocha, Pierre Lechantre kufanya mabadiliko ya kumtoa beki Juuko Murushid, na nafasi yake ikichukuliwa na Mshambuliaji, Mburundi, Laudit Mavugo.

Simba ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 66 ya kipindi cha pili baada ya mpira wa kona kumfikia Mavugo ambaye aliumalizia kwa mguu na kufanya matokeo mpaka dakika 90 zinamalizika yaende sare ya 1-1.

Matokeo hayo yameipa Simba alama moja na kuifanya ifikishe pointi 59 kwenye msimamo wa ligi.

2 COMMENTS:

  1. Lipuli walikamia kama kawaida hizi timu kama zingekuwa zinacheza kama hivi kwa mechi zao zote basi mpira wa Tanzania ungekuwa. Lakini inaonekana wachezaji wa timu nyingi hasa za mikoani hutaka kuonekana wanapocheza na simba, Yanga au azam halafu mechi nyengine wachezaji wanakuwa nyanya.Angalia timu kama Mbao au stand United.

    ReplyDelete
  2. Mpira wa Tanzania hauwezi kukua kwa kukamia timu kubwa tu, mbona wanafungwa na timu ndogo sasa mpira utakuwa namna gani? Badilikeni au mnacheza ili kusajiliwa na timu kubwa tu?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic