Na George Mganga
Yanga imepangwa kwenye kundi hilo ikiwa na timu za USM Alger ya Algeria, Rayon Sports ya Rwanda pamoja na Gor Mahia FC ya Kenya.
Ratiba inaonesha kuwa Yanga itaanza kucheza na USM Alger ugenini Mei 6 2018, kabla ya kuvaana na Rayon Sports Mei 16 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Baada ya michezo hiyo, Yanga itakuwa mgeni dhidi ya Gor Mahia FC ambapo mechi itapigwa Nairobi Julai 18 2018, kisha baada ya hapo itakuwa mwenyeji dhidi ya Gor Mahia FC tena Julai 29 2018.
Ratiba hiyo inaonesha baada ya kukipiga na Gor Mahia, Yanga itawakaribisha USM Alger Uwanja wa Taifa Agosti 19 2018, kisha itasafiri kuelekea Rwanda kukabiliana na Rayon Sports Agosti 29 2018.
Salehjembe.blogspot.com inaitakia kila la kheri Dar es Salaam Young Africans kuelekea michezo hiyo ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho.
Kwa kundi hili, Yanga washindwe wenyewe.
ReplyDeleteDuuh jamaa wanazidi kupata zari la mental..😎😎😎
Delete