April 3, 2018



Na George Mganga

Simba imezidi kujiweka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara jioni ya leo baada kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Njombe Mji FC.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Sabasaba, Simba walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Nahodha wake, John Bocco, aliyefunga kwenye dakika ya 14 ya mchezo kwa shuti kali la kushoto, nje kidogo ya eneo la 18.

Baada ya bao hilo, Njombe Mji walionesha kuamka zaidi wakionesha kupambana kutafuta bao la kusawazisha huku wakimiliki mpira kwa wingi kuliko Simba, lakini juhudi zao hazikuzaa matunda ambapo mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika, matokeo yalikuwa ni 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kasi kwa timu zote mbili kushambuliana kwa zamu, lakini baadaye mnamo dakika ya 64, Shomari Kapombe alipata mpira pembezoni kulia mwa Uwanja na kumtengenezea Bocco ambaye bila ajizi alipasia kambani mpira, na kuifanya Simba iwe mbele kwa mabo 2-0.

Katika mchezo huo, Kiungo Haruna Niyonzima na beki Mbonde waliingia kipindi cha pili wakichukua nafasi za Emmanuel Okwi na James Kotei. Mbode na Niyonzima walikosekana dimbani kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi.

Matokeo hayo yanaifanya Simba ifikishe jumla ya pointi 49 na kuiacha Yanga iliyo na 46 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo sawa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic