April 7, 2018




Ingawa machoni inaonekana kiroho kinamdunda, lakini Mfaransa wa Simba,Pierre Lechantre amewaambia mashabiki kwamba hana wasiwasi kabisa na mechi ya Mtibwa itakayopigwa Jumatatu mjini Morogoro.

Simba kwa sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 49, ambazo ni tatu zaidi ya Yanga inayoshika nafasi ya pili nyuma ya Azam inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 44 huku ikiwa mbele kwa mchezo mmoja.

Simba imefikisha ponti hizo baada ya kupiga mabao 2-0 katika mechi yake ya kiporo dhidi ya Njombe Mji iliyopigwa Jumanne iliyopita.

Lechantre ambaye CV yake ni kubwa kuliko makocha wote walioko kwenye Ligi Kuu msimu huu anasema; “Binafsi pamoja na wachezaji wangu hatuna presha ya mchezo huo kwa sababu kikubwa tunachokitaka ni kuona tunafunga mabao ya kutosha katika mchezo huo ili kuendelea kuwa karibu na ubingwa hilo ndiyo kubwa kutokana na kasi ya wapinzani wetu lakini nataka kushinda kila mchezo uliopo mbele ndiyo jambo la msingi.”

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic