Simba na Yanga zinakutana leo ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili ya ligi kufuatia ule kwa kwanza timu hizo kwenda sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mkapa amesema kuwa mechi hii huwa si rahisi kutabirika kutokana na upinzani wa aina yake namna unavyokuwa kwa timu hizi mbili.
Akizungumza kupitia Radio EFM kwenye kipindi cha Michezo, Mkapa ameeleza kuwa Yanga inaweza ikapata matokeo leo kutokana na namna wachezaji wa Yanga walivyojipanga.
Beki huyo aliyewahi kuichezea Yanga, amesema Simba wataingia wakiwa wamejiamini kufuatia uzuri wa matokeo waliyonayo msimu huu.
Kutokana na kuonesha kiwango kizuri tangu msimu huu uanze, Mkapa anaamini Yanga watahitaji kuimaliza Simba leo ili ijitengenezee mazingira mazuri pengine inaweza ikautwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.








Kwa taarifa yako...upande utaokapata shida katika mechi ya leo ni ule anaocheza Gadiel Michael kwa upande wa Yanga ambapo ndipo anapopita Okwi na Agey...Ila upande wa Asante Kwasi pia utakuwa wa moto kwani ndipo anapopita Muhilu na Kessy. Ila 3-5-2 isipotumika vizuri gharama yake itakuwa kubwa maana kama Okwi asipokuwa anamsaidia Agey itakuwa shughuli upande huo
ReplyDelete