April 29, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga umetaja rasmi sababu ya wao kujiita wa Kimataifa, neno ambalo liliasisiwa na aliyewahi kuwa Msemaji wa timu hiyo, Jerry Muro.

Kupitia Afisa Habari wa sasa, Dismas Ten, ameeleza kuwa wao wanajiita wa kimataifa sababu wanaujua umuhimu wa mashindano hayo na hivi sasa wapo kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ten amesema wao wanajua umuhimu wake hivyo ni vema wakayetendea haki kwa maana wanatarajia kuanza kibarua chao dhidi ya U.S.M Alger ya Algeria.

Yanga inatarajia kuondoka nchini kuelekea Algeria siku kadhaa zijazo baada ya mchezo dhidi ya Simba kumalizika leo.

4 COMMENTS:

  1. Mawazo ya Ten hayavuki ulefu wa pua yake,mwisho wa msimu aje atuambie klabu inayojuwa umuhimu wa mashindano ya kimataifa mwakani itashiriki mashindano gani?

    Labda MAPINDUZI CUP kwa kuwa hufanyika "nchi jirani ya Zanzibar"

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama mwakani hawashiriki hakuwaondolei kuwa wa kimataifa Bali kumesaidia wengine kujifunza na kujitoa huko kwenye jina lao.

      Delete
    2. Kama mwakani hawashiriki hakuwaondolei kuwa wa kimataifa Bali kumesaidia wengine kujifunza na kujitoa huko kwenye jina lao.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic