MCHEZAJI YANGA AKUMBUSHIA SIMBA WALIVYOINUSURU KUSHUKA DARAJA, NI MIAKA 30 IMEPITA
Homa ya mchezo wa watani wa jadi unaopigwa majira ya saa 10 kamili jioni katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo jioni inazidi kushika kasi na kuteka hisia za watu.
Wakati mashabiki na wadau mbalimbali wakitoa utabiri wao kuelekea mechi hii, mchezaji wa zamani wa Yanga, Kenneth Mkapa, ameitabiria Yanga kupata matokeo dhidi ya Simba.
Mbali na utabiri huo, Mkapa amekumbushia namna walivyoinusuru Simba kushuka daraja mwaka 1987/88 kufuatia sare ya bao 1-1.
Mkapa ameeleza kupitia radio EFM kuwa msimu huo Simba hawakuwa vizuri na hata katika mchezo huo mwishoni mwa msimu walidhamiria kuifunga Simba lakini matokeo yakawa tofauti na kwenda sare ya bao 1-1.
Leo hii Simba inashuka Uwanjani ikiwa mwenye wa pambano dhidi ya Yanga ambapo ni zaidi ya miaka 30 tangu kunusurika kushuka daraja.
Kaishiwa hoja. Miaka 30 ndio umri wake sasa hiyo ya kukumbushia leo ? Wahamasishe wachezaji wako washinde leo. Historia ya magoli 6-0, 5-0 mbona husemi?
ReplyDelete