April 25, 2018



Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amewapiga kijembe 'UTANI' watani zake wa jadi Simba kuhusiana na kambi waliyoweka Morogoro.

Akizungumza na Radio EFM kupitia kipindi cha Michezo 'E Sports', Mkwasa amesema kuwa inawezekana Simba wameweka kambi Morogoro kutokana na kuyumba kiuchumi.

Mkwasa vilevile ameeleza kuwa yawezekana Simba wameshindwa kwenda Zanzibar kuweka kambi huko kutokana na gharama kuwa kubwa, hivyo nao wamemua kuwa Morogoro.

Kijembe amewapiga Simba zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya mtangange dhidi yao kupigwa Uwanja wa Taifa, Jumapili ya Aprili 29 2018.

3 COMMENTS:

  1. Hahahaa. Huyu jamaa anachekesha sana. Wao ndio waliojengeka kiuchumi, kwani si inajulikana mishahara mitatu ilikuwa haijalipwa na moja ndio sababu ya kocha wenu kukimbia na Plujin kutaka alipwe chake ndio afikirie kurudi

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...huyu nae ni goroka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic