April 25, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga umeweka wazi kuhusiana na suala la Kocha wake, Mkongomani, Mwinyi Zahera, kuanza kazi ndani ya timu yao.

Katibu Mkuu wa klabu, Boniface Mkwasa, amefunguka kwa kueleza ni mapema mno kwa sasa kulizungumzia hilo kutokana na taratibu ambazo bado zinapaswa kukamilika.

Mkwasa ameeleza kuwa kuna mambo mbalimbali ya kufuata ikiwemo kibali cha kazi ukizingatia yeye bado ni mgeni ndani ya taifa hili, hivyo vema wakalikamilisha kwanza.

Mbali na hilo, Mkwasa amesema kuwa Zahera anaweza akaukosa mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumapili ya wiki hii.

Zahera aliwasili nchini jana kuja kumalizana na Yanga kwa ajili ya kuanza kibarua rasmi cha kuanza kuinoa Yanga ambayo iliondokewa na Kocha wake Mkuu, Mzambia George Lwandamina.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic