April 1, 2018







Msanii maarufu wa India, Aliyah ambaye ameigiza Tamthilia ya Beintehaa, kesho Jumapili anatarajia kuwa mgeni maalumu katika Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) zinazotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mliman City jijini Dar.


Akizungumza na waandishi wa habari, Aliyah alisema kuwa, amefurahi kuwa mmoja wa wageni waalikwa wa tuzo hizo.


“Nimetembea nchi nyingi kutokana na kazi yangu hii, nimefurahi kuwa mgeni katika tuzo hizi hapa Dar, niwaambie tu wasanii wakijituma wanaweza kufika mbali kama mimi.

“Siri ya mafanikio ya kuwa msanii mkubwa ni kutokana na kuipenda kazi hii. Mbali ya kuwa muigizaji, pia naweza kuimba na kuandika filamu,” alisema Aliyah.


Katika hatua nyingine, muandaaji wa tuzo hizo, Zamaradi Nzoa, alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mablimbali wa serikali akiwemo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harryson Mwakyembe.


“Mbali na hao, pia wasanii mbalimbali na waigizaji wanatarajia kuwepo ambao ni Diamond, Ommy Dimpoz, Wema Sepetu, Hamisa Mobetto na wengineo,” alisema.

Katika tuzo hizo, vipengele 19 ndiyo vitakavyoshindaniwa ambapo kila mshindi atapata tuzo na pesa taslimu ambapo jumla ya shilingi milioni 41 zitatolewa kwa washindi.


Tuzo hizo zitaenda sambamba na uzinduzi wa vipindi vipya vya sinema zetu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic