April 25, 2018



Uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar FC umesema hauna wasiwasi na ushiriki wao katika mashindano ya kimataifa endapo wanatafinikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United.

Kupitia Msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru, ameeleza hawana wasiwasi sababu adhabu yao imeshamalizika hiyo hakuna shaka kwenye ushiriki wao.

Kifaru anaamini kila kitu kitakuwa sawa kutokana na baadhi ya taarifa zinazoelewa kuwa inawezekana ikawa ngumu kupata nafasi hiyo baada ya kufungiwa na CAF miaka iliyopita.

Mtibwa na Singida United ndizo timu zilizotinga kuingia hatua ya fainali ya Kombe la FA ambapo zitakutana June 2 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic