April 9, 2018


FULL TIMEDakika ya 90+ 3: Mwamuzi anamaliza mchezo.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 89: Niyonzima anapiga shuti linadakwa na kipa wa Mtibwa. 
Dakika ya 85: Mchezaji wa Simba yupo chini, mchezo umesimama, anatibiwa huku wengine wakiendelea kujadiliana.
Dakika ya 84: Mtibwa wanapiga shuti linafdakwa na Manula.
Dakika ya 84: Mtibwa wanalishambulia lango la Simba kwa kasi.
Dakika ya 80: Mtibwa wanamiliki mpira, Simba wanajaribu kuwavuruga.
Dakika ya 76: Simba wanamtoa Asamoh Gyan anaingia Haruna Niyonzima.
Dakika ya 73: Mtibwa wanafanya mabadiliko, Dilunga anatoka, anaingia Semtawa.
Dakika ya 72: Hassan Mganga anapiga inagongwa kichwa lakini Manula anauwahi mpira na kuudaka.
Dakika ya 71: Mbonde anacheza faulo, mwamuzi anapuliza filimbi. Anapewa kadi ya njano.
Dakika ya 69: Shangwe ni kubwa, Mtibwa wanacheza kwa kujiamini kwa sasa.Dakika ya 66: Kocha wa Simba, Pierre Lechantre analalamika kwa mwamuzi wa akiba akiwa amelowa.
Dakika ya 58: Simba wanarudi nyuma na kujipanga, kasi ya Mtibwa unaongezeka.
Dakika ya 52: Simba wanashambuliwa, Manula anafanya kazi nzuri ya kutoa michomo kadhaa.
Dakika ya 47: Kasi ya mchezo siyo kubwa.

Kipindi cha pili kimeanza.

Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.
Mapumziko

Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.
Dakika ya 45 + 3: Mchezo unaendelea.
Mchezo umesimama kwa muda.
Dakika ya 45 + 1: Okwi anaingiaa na mpira, anapiga shuti kipa wa Tinoko anadaka lakini anaumia.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 40: Timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 37: Mtibwa wanapata kona mbili mfululizo.
Dakika ya 35: Simba wanapata kona, ni baada ya beki wwa Mtibwa kuutoa mpira.
Dakika ya 30: Kocha wa Mtibwa amesimama, anatoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Dakika ya 28: Mtibwa wanapata kona, inapigwa inaokolewa, inakuwa goal kick.
Dakika ya 27: Mchezo umesimama kwa muda, wachezaji wa Simba wanapeana maelekezo.
Dakika ya 23: Shangwe zimeongezeka uwanjani.
Kichuya anapiga krosi, inatua kichwani mwa John Bocco, anapiga kichwa kisha Emmanuel Okwi anamalizia kwa ulaini. Simba wanapata bao.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOODakika ya 23: Mvua inaendelea kunyesha uwanjani.
Dakika ya 21: Mtibwa wanacheza faulo, Mzamiru anapiga lakini walinzi wa Mtibwa wanaokoa.
Dakika ya 18: Kipa wa Mtibwa Tinoko anaonyesha umahiri wa kumiliki mpira.
Dakika ya 15: Mtibwa wanaonyesha kujiamini na kupiga pasi kadhaa, wanashangiliwa na mashabiki wao.
Dakika ya 10: Mvua imeanza kunyesha mdogomdogo kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Dakika ya 5: Simba wanamiliki mpira lakini Mtibwa wanaonyesha kuwa makini.
Dakika ya 4: Kipa wa Mtibwa yuko chini anapatiwa matibabu baada ya kuumia.
Dakika ya 1: Kasi imeanza taratibu.Mchezo umeanza.
Idadi ya mashabiki ni wengi uwanjani hapa.

Huu ni mchezo wa Ligi Kuu Bara, unaotarajiwa kuanza muda si mrefu kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

4 COMMENTS:

  1. Lazima walie mtibwa hilo lipo wazi.

    ReplyDelete
  2. matokeo yako hayaendi na mda mbona salehe

    ReplyDelete
  3. Dk 76 Simba wanamtoa Asamoah Gyan anaingia Haruna Niyonzima,waandishi wetu mnazidi kutupotosha jamani andikeni kwa usahihi ili tuthamini mchango wenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic