April 20, 2018



Baada ya kusonga mbele mpaka hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Mjumbe Mkongwe wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, ametoa pongezi kwa klabu yake.

Akilimali amewasifu vijana wake kwa namna walivyopambana kuhakikisha wanafuzu kuingia hatua hiyo kutokana na kuiondosha Wolaita Dicha SC.

Mjumbe huyo ameelezea furaha yake kwa wachezaji wa kikosi hicho huku akisema bado wanahitaji kushikwa mkono ili wajitume zaidi haswa kuelekea mechi zingine zitakazofuata.

Kikosi hicho kimewasili usiku wa leo jijini Dar es Salaam na kupokelewa na baadhi ya mashabiki katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Yanga imefuzu kuingia hatua hiyo kwa idadi ya mabao 2-1, ambapo katika mechi ya mkondo wa pili ilikubali kufungwa bao 1-0 Aprili 18 wiki hii huko Awassa, Ethiopia.

1 COMMENTS:

  1. kati ya vitu huwa vinakera ni jinsi hawa wazee especially mzee Akilimali anavyopewa airtime na media za Kitanzania ilhali tuikjua hawa ni sehemu ya kuharibu maendeleo ya timu zetu pendwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic