MKWASA AGEUKA MBOGO KUHUSIANA NA MILIONI 600 ZA CAF, AZIWEKEA MSISITIZO HUU
Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amewapa salaam wale wote wanaozitolea macho fedha za Yanga ambazo wamezitwaa kufuatia kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga itapokea kiasi cha zaidi ya milioni 600 baada ya kuiondosha Wolaita Disha SC kwa idadi ya mabao 2-1.
Mkwasa amesema fedha hizo zitakuwa ni maalum kwa ajili ya Yanga pekee na si watu wengine wanaopanga kuzitumia kimaslahi binafsi.
Katibu huyo amesisitiza ni lazima fedha hizo zitumike ndani ya klabu ukilingana na wakati ambao Yanga hivi sasa inapitia.
Baada ya kufuzu kuingia hatua hiyo ya makundi, Yanga inasubiri droo ambayo inafanyika kesho kuona itapangwa kucheza na nani ikiwa ni hatua ya kuelekea nane bora.
Haya tutaona
ReplyDelete