April 26, 2018



Mwanachama aliyesimamishwa na uongozi wa klabu ya Simba kufuatia sekeseke la kufungua kesi mahakamani kupinga mabadiliko, Mzee Hamis Kilomoni, ametoa nasaha zake kwa Simba kuelekea mechi dhidi ya Yanga Jumapili hii.

Kilomoni ameeleza kuwa mechi hiyo haitokuwa rahisi japo amesema kuwa wana kikosi kipana kitakachowasidia kupata matokeo.

Mzee huyo ambaye hivi karibuni aliingia kwenye rada za Simba kutokana na kupinga mabadiliko ya timu hiyo kuingia katika mfumo wa kisasa kiuendeshwaji, ana imani timu yake inaweza kufanya vizuri japo akikiri kuwa mechi itakuwa ngumu.

Kilomoni anaamini Simba inaweza kushinda endapo wachezaji wataweza kupambana bila kuonesha hali ya kujiamini zaidi Uwanjani.

Mjumbe huyo wa zamani wa Baraza la Wadhamini ndani ya Simba, ameeleza kuwa timu zote ni kubwa wala haitahitajika kuichukulia mzaha Yanga ambayo haijawa na matokeo mazuri kama Simba msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic