April 26, 2018



Baada ya kuwasili jana mjini Morogoro na kupata nafasi ya kukinoa kikosi cha Yanga kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia, jezi ya Kocha Mkongomani Mwinyi Zahera yawa gumzo kwa baadhi ya mashabiki wa timu zote mbili.

Zahera alitinga Uwanjani kuishuhudia timu yake mpya akiwa amevalia uzi mweusi wenye micharazo ya rangi nyekundu kwenye mabega, rangi ambayo haijawahi kutumika kabisa katika klabu hiyo yenye maskani yake katika mitaa ya Twiga, iliyo Jangwani, Kariakoo.

Baadhi ya mashabiki ikiwemo wale wa Yanga na Simba, wamekuwa wakihoji imekuwa avae rangi ambazo hazitumiki ndani ya klabu.

Wapo wale walioandika mitandaoni haswa wa upande wa pili wakitupa vijembe kuwa Mkongo huyo ana damu ya Simba kutokana na rangi hiyo nyekundu.

Rangi ya Yanga ambayo inatambulika siku zote ni kijani na njano, pia hivi karibuni wamekuwa wakitumia nyeusi haswa katika mechi za ugenini.

Kitendo cha Zahera kuvaa rangi hiyo ambayo hutumiwa na watani zao wa jadi Simba, imekuwa gumzo kubwa zaidi kwa baadhi ya mashabiki ambao hawajawahi kuiona ikitumika Jangwani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic