Ruvu Shooting imepoteza mchezo wake wa ugenini kwa kuchapwa mabao 3-1 na wenyeji wao Majimaji.
Baada ya kipigo hicho, maana yake Majimaji “imeipapasa” Shooting kama ambavyo Msemaji wao, Masau Bwire amekuwa akitumia hilo neno.
“Pamoja na taarifa kuenea mitandaoni, kwamba Ruvu Shooting, wamepapaswa, Masau ameibuka na kutoa sababu huku akisema walitegewa miba.
Tambueni Majimaji Sc hawana maarifa wala uwezo wa kuipapasa Ruvu Shooting ila, walizuia sehemu zote za kupapaswa kwa kuweka miba,” anasema Masau na kuongeza.
“Hatukupapaswa, tumeshindwa kupapasa kutokana na "miba" kuwekwa maeneo ya kupapaswa! Bila akili kubwa, ni vigumu kutambua!”
0 COMMENTS:
Post a Comment