April 4, 2018




Taarifa kutoka ndani ya Azam FC zinaeleza kuwa mchezaji, beki, Daniel Amoah anaweza akakosekana nje ya Uwanja wa muda wa miezi 9.

Amoah alipelekewa Afrika Kusini katika hospotali ya Vincent Pallot, Cape Town, kufanyiwa matibabu ya goti ambalo aliumia takribani miezi miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa Daktari wa timu kutoka Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, ameeleza kuwa Amoah alikutwa na tatizo kubwa kwenye goti lake na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji kesho Alhamis ambao utamfanya akae nje ya Uwanja kwa muda wa miezi 9. 

Mbali na Amoha, Mshambuliaji wa timu hiyo pia Wazir Junior naye anasumbuliwa na maumivu ya enka ambayo yamemfanya akosekane dimbani kwa mechi kadhaa, pia anaendelea na matibabu hivi sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic