April 4, 2018





Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya imeendelea usiku wa kuamkia jana kwa mechi mbili kuchezwa.

Juventus iliyokuwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani iliambulia kichapo cha mabao 3-o kutoka kwa Real Madrid huku Ronald akiibuka shujaa kwa kupachika mabao mawili.

Mchezo huo wa raundi ya kwanza unaitengenezea mazingira mazuri Real Madrid kusonga mbele hatua ya nusu fainali endapo italinda matokeo yake katika mzunguko wa pili.

Bao jingine la Real Madrid lilifungwa na Marcelo katika mchezo huo.

Mbali na Madrid, Sevilla waliondoa Manchester United 16 bora jana walichezea kichapo cha mabao 2-1 wakiwa kwao Spain dhidi ya Bayern Munich.

Mabao ya Munich yalifungwa na Jesus Navas pamoja na Thiago Alcantara huku bao pekee la Sevilla likifungwa na Sarabia.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic