April 24, 2018



Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Rivaldo, amemtaka Neymar Junior kuachana na PSG ya Ufaransa kama anataka kuwa bora.

Rivaldo amefikia hatua hiyo ya kumshauri Neymar kutokana na kukosa furaha tangu ajiunge na wababe hao wa ligi ya Ufaransa.

Mbrazil huyu amemwambia Neymar kuwa, endapo kweli anahitaji kuwa mchezaji bora duniani, ni vema akaondoka kwa matajiri hao ili akatafute maisha mengine nje ya Ufaransa.

Neymar amekuwa akihusishwa kurejea tena Barcelona kutokana na uhaba wa mataji ndani ya PSG. Taarifa za kuhitaji kurejea Barcelona zilishika kasi baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic