April 29, 2018



Na George Mganga


Bao pekee la Erasto Nyoni limeipa Simba ushindi dhidi ya watani zao wa jadi Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.

Nyoni alifunga bao hilo katika dakika ya 37 kwa kichwa, kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa kushoto mwa Uwanja na mshambuliaji Shiza Kichuya.

Katika mchezo huo mashabiki wa Simba wlaijitokeza kwa wingi zaidi ya wale wa Yanga huku wakijitoa kuishangalia zaidi timu yao wakati wote.

Dakika 90 za mchezo mzima zimemalizika kwa Yanga kushindwa kupata kona hata moja wakati huo Simba wakipata kona 8.

Beki Hassan Kessy alitolewa nje mnamo kipindi cha pili kwa kadi ya pili ya njano na nyekundu kutokana na kitendo cha kumchezea faulo, Asante Kwasi.

Matokeo hayo yanaifanya Simba izidi kujiweka kileleni kwa kufikisha jumla ya alama 62 huku Yanga ikisalia na 48.


2 COMMENTS:

  1. Inaonesha wazi yule kocha Mzambia Luandamina alijuwa mapema kuwa Yanga itachezea kichapo na ili kujinusuru na akaamuwa kuingia mitini kujinusuru na aibu na uwezekano wa kufukuzwa

    ReplyDelete
  2. Na ingelikuwa si papala za washambuliaji wa mnyama basi yanga wangelichapwa hata magoli mane. wamemvunja moyo kocha wao mpya aliefika kuonesha uwezo wake mkubwa. Yalabi salalama asije na kuingia mitini kwasababu bado zipo timu tatu ngumu za kuchezea ugenini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic