April 6, 2018




Mziki umekamilika! Hivi ndivyo utakavyoweza kusema ni baada ya washambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe na Yohana Nkomola kujiunga na kambi ya pamoja Mkoani Morogoro.

Wachezaji hao wameungana na kambi hiyo kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Walayta Dicha FC ya nchini Ethiopia utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Washambuliaji hao walikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu wote wawili wakisumbuliwa majeraha ya goti yaliyowasababisha kuzikosa mechi za Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema washambuliaji hao walitua na kujiunga na kambi hiyo tangu Jumatatu ya wiki hii na kuanza kufanya na mazoezi mepesi ya binafsi kabla ya kuanza magumu na wenzao.
Saleh alisema, kurejea kwa washambuliaji kutaimarisha kikosi chao ambacho kitamkosa mshambuliaji wake Mzambia, Obrey Chirwa kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano alizozipata katika michezo iliyopita.

“Ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga kuwa mshambuliaji wao kipenzi, Tambwe amepona na ameanza mazoezi magumu na wenzake baada ya kupona majeraha ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja muda mrefu.

“Pia, Nkomola naye amepona na walijiunga pamoja na Tambwe kambini kwetu Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Dicha, hivyo kurejea kwao kikosi kutaimarisha kikosi chetu.

“Kama unavyofahamu katika mechi hii tutamkosa Chirwa mwenye adhabu ya kadi, hivyo kurejea kwao kutamfanya kocha kuchagua mchezaji yupi amtumie atakayesaidiana na Ngoma (Ngoma) ambaye yeye naye amerejea na kuanza mazoezi muda mrefu na timu,”alisema Saleh.

1 COMMENTS:

  1. Ili washinde list ni hii
    1. Rostand 2.Abdul 3.Mwinyi 4. Andrew 5. Nadir 6. Kamusoko 7. Kesi 8.Daudi 9.Mahadhi 10. Ajib 11. Gadiel

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic