April 7, 2018



Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoa maamuzi ya rufaa iliyokatwa na aliyekuwa Makamu wa Rais shirikisho hilo jana kupitia Kamati ya Maadili, Michael Wambura, Wambura ameibuka leo kusema hayakuwa sahihi.

Wambura amesema kuwa maamuzi hayo hayakuwa sahihi na hivyo hakubaliani nayo kwa namna ambavyo yalitolewa.

Licha ya hilo, Wambura ameeleza kuwa Kamati ya Maadili imeleta majibu ambayo ni ya kishabiki huku akidai kilichofanyika wakati wa usikilizwaji wa rufaa na maamuzi yaliyotoka ni vitu viwili tofauti.

Kuafuatia majibu ya rufaa hiyo, Wambura ataendelea kutumikia adhabu yake ya kifungo cha kutojihusisha na masuala ya soka, huku kamati ikieleza kutupilia mbali rufaa ya Wambura jana.

1 COMMENTS:

  1. Michael Wambura...sikia ni miongo miwili hii nikimaanisha karibia miaka ishirini tunakusikia wewe na kushatakiana na FAT mara Simba hadi ikaingia TFF.Tokea enzi za kina Muhidini Ndolanga, Tenga na sasa kina Karia.Kulikoni? Mbona umekuwa king'ang'anizi hivyo? Nenda mahakamani uksafishe jina lako kama wanakuonea.Kwani Wambura hakuna maisha nje ya TFF au soka?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic