April 8, 2018



Na George Mganga

Kufuatia kukosekana katika mchezo wa Kombe la Shirikisho jana dhidi ya Wolaitta Dicha FC kutoka Ethiopia, wachezaji Papy Kabamba, Obrey Chirwa, Kelvin Yondan na Said Makapu watakuwepo kwenye mchezo wa marudiano.

Wachezaji hao ambao wamekuwa mhimili mkubwa wa kikosi cha Yanga kwa msimu huu, walishindwa kutumika jana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano kwa kila mmoja.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), liliwatumia barua Yanga kuelekea mechi hiyo likiwakumbushia kutowatumia wachezaji hao sababu ya kadi hizo za njano.

Tayari wameshamaliza adhabu hiyo waliyoitumikia jana, sasa watakuwa chachu ya kuongeza nguvu kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Ethiopia wiki moja baadaye.

Yanga itaondoka nchini katikati ya wiki kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya mkondo wa pili.

Kikosi hicho kitahitaji sare ama suluhu ama ushindi wa aina yoyote ile ili kusonga mbele kuingia hatua ya makundi.

1 COMMENTS:

  1. haitakua game rahisi lakini naamini tutavuka na kuingia hatua ya makundi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic