Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amepewa fursa kuwa mkufunzi tajiri zaidi duniani iwapo atajiunga na ligi kuu ya China.(Mirror)
Wenger ameombwa kuchukua wadhfa wa meneja mkuu katika klabu ya PSG(Le10 via Talksport)
Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa kipa David de Gea hataondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu.
De Gea 27 anakamilisha mwaka wake wa mwisho wa kandarasi yake lakini United ina chaguo la kuongeza mwaka mwengine na wanajiandaa kwa mkataba mpya. (Manchester Evening News)
Mshambuiaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 27, anasema kuwa ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu hatma yake ya siku zijazo. Amehusishwa na Barcelona na Manchester United (Sun)
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola yuko tayari kumzuia Mikel Arteta kusalia miongoni mwa makocha wake licha ya raia huyo wa Uhispania kuhusishwa na Arsenal. (Mirror)
Kocha wa Chelsea Antonio Conte huenda akakosa wadhifa wa kuinoa wa timu ya taifa ya Italy. Conte mwenye umri wa miaka 48 anataka mkataba mpya wa miaka mitano lakini shirikisho la soka nchini humo limekataa kupokeaa mahitaji hayo.(Times)
Imeandaliwa na BBC.
Imeandaliwa na BBC.
0 COMMENTS:
Post a Comment