YANGA WAPATA MWALIKO KUTOKA KWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ETHIOPIA, WAPIGA MSOSI WA MAANA
Kikosi cha Yanga kimejumuika na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Naimi S. Aziz, kupata mlo wa mchana mjini Addis Ababa.
Yanga walipata mwaliko kutoka kwa Balozi huyo baada ya kusonga mbele kunako mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kutinga hatua ya makundi.
Balozi Aziz ameona awaalike Yanga nyumbani kwake kuwapa faraja kutokana na kushindwa Uwanjani kuwatazama wakicheza dhidi ya Wolaita Dicha, sababu ya majukumu ya kikazi.
Timu hiyo imeondoka mchana huu hapo Addis Ababa kuanza safari ya kuja Tanzania ambapo kinatarajiwa kuwasili majira ya saa 7 usiku.
0 COMMENTS:
Post a Comment