April 10, 2018



Wakati Singida United ikiwa katika maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Yanga kesho, Uongozi wa timu hiyo wasema kile kipigo ilichofungwa na Simba mzunguko wa kwanza kilikuwa cha mipango.

Kupitia Mkurugenzi wa timu hiyo, Festo Sanga, amesema kuwa wameamua kuweka kambi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ili kuepuka kilichowatokea Uwanjani kama ambavyo Simba waliwafanyia.

Akizungumza na kipindi cha michezo kupitia Radio Magic, Sanga ameeleza kuwa wakati wanakuja kuweka kambi fupi wakati ligi ikiwa kwenye mzunguko wa kwanza, Simba waliwafanyia fitina.

Sanga amesema Simba inawezekana waliwahujumu wachezaji wao kwa kuwapiga milungula kitu ambacho kilisababisha Singida ifungwe kwa idadi hiyo ya mabao 4-0.

Kutokana na tukio hilo kutokea, Singida wameamua kujificha nje ya mji wa Dar es Salaam ili lisiweze kujirudia kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Yanga.

7 COMMENTS:

  1. ANAJITAMBUA KWELI HUYU? nasubiri povu la Manara

    ReplyDelete
  2. Hujitambui wewe juzi tu mmepigwa 3 na Mtibwa ila mkifungwa na Simba ooh wachezaji wamepewaa pesa jaribuni kuwa wa kweli na kukubali vichapo bana

    ReplyDelete
  3. Hivi kiongozi kama huyu bado achukuliwi hatua na mamlaka za soka na serikali?

    ReplyDelete
  4. Hivi kiongozi kama huyu bado achukuliwi hatua na mamlaka za soka na serikali?

    ReplyDelete
  5. Kichaa huyo. Mtibwa walimpa yeye mlungula sasa.

    ReplyDelete
  6. kwenu mtibwa amewapiga tatu bila itakuwa ugenini suburi tano za yanga leo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic