April 18, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kimefanikiwa kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Africa baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Wolaita Dicha SC kutoka Ethiopia.

Yanga imefuzu kuingia hatua hiyo kutokana na faida ya ushindi wa nyumbani ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Wolaita Dicha walianza kwa kasi mpambano wa leo kwa kulisakama lango la Yanga na kufanikiwa kupata bao la mapema, mnamo dakika ya pili ya mchezo.

Ushindi huo umeiwezesha Yanga kutwaa kitita cha zaidi ya milioni 600 za kitanzania kufutia kuiondosha Dicha kwenye mashindano.

Mbali na mpunga huo, ushindi huo unakuwa kama salaam kuelekea mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba itakayopigwa Aprili 29 2018 kwenye Uwanja wa Taifa.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Yanga itaanza safari ya kurejea nchini kesho ili kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City FC.

8 COMMENTS:

  1. Ushindi au kipigo? Sema wamevuka, sio ushindi huo ni salam kwa simba. Tunawasubiri

    ReplyDelete
  2. Mwandishi ovyoo....salaam kwa Simba kwa vipi? Yanga inasubiri kipigo kama alichopewa leo na hawo Waethiopia au nakuelewa vipi?

    ReplyDelete
  3. Tena sio kipigo kidogo,kipigo cha maana wakapumzike mbele ya safari.

    ReplyDelete
  4. Huyu mwandishi huwa anafurahisha sana habari zake kwann sionsalaam kwa Mbeya city?

    ReplyDelete
  5. Kwa faida yenu mwandishi hajakosea mechi hizi mpira ni dakika 180, 90 nyumbani na 90 ugenini..kami imepigwa kwanini iendelee na mashindano?

    ReplyDelete
  6. Ewe muandishi wee mbona unatuchefuwa roho, salamu gani hizo kwa Simba ambapo hiyo yanga yako imeondoka kwa kichapo? Huo hauitwi ushindi na hizo pesa walizopata haki ya Mungu kama tusi kwa yanga, kwahivo hawasherehekei ushindi na huku wamefungwa bali wanasherehekea pesa zinazowasuta

    ReplyDelete
  7. Masokini roho zao yanga, eti mabosi wao matajiri watawapa mamilioni ya shilingi baada kipigo Hawa nahuku wakikosea chupuchupu.Eti wamecheza kwa morali juu. Huku huyo Canavaro wao akitamka waziwazi kwakusema bila ya kuona aibu kuwa Simba haiwanyimi usingizi PESA ndio muhimu kwao. Aibu tupuu. Ati salamu kwa Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic