Monaco yaangalia kumchukua kiungo
kutoka Ufaransa Thomas Lemar msimu wa majira ya joto. Timu za Arsenal na
Liverpool pia zimeonekana kumtupia jicho Mfaransa huyo mwenye umri wa
miaka 22.(Telefoot)
Aliyekuwa mchezaji wa West Brom,Derek McInnes na mkuu wake wa Baggies Tony Mowbray ni miongoni mwa waliopendelewa kupata kazi ya kuwa meneja wa West Brom (Mirror)
Rais wa Roma James Pallotta anasema klabu hio 'haina nia ya kumuuza' mlinda mlango kutoka Brazil Alisson(25), ambaye ana aminiwa kuhamia Liverpool.
Mlinzi wa Chelsea Antonia Rudiger, 25, anasema hajajua sababu ya yeye kutocheza dhidi ya Southampton, akiongezea kuwa alikuwa 'tayari kabisa' kwa ajili ya mechi ya Jumamosi.
Newcastle wanajipanga kumsajili mlinda mlango Martin Dubravka kwa mkataba endelevu. Mslovak huyo,29, aliungana na Magpies kwa kukopeshwa na timu ya Sparta Prague mwezi Januari. (Express)
Mkuu wa Newcastle Rafael Benitez anatarajia kufanya mazungumzo na mmiliki wa timu, Mike Ashley kabla ya kusaini mkataba mpya . Benitez anataka kuhakikisha kuwa kuna fedha za kutosha za kufanyia usajili wa wachezaji katika msimu wa majira ya joto kabla ya kuingia katika klabu hio.(Telegraph)
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema anajutia kwamba hakuweza kumshawishi winga wa Eagles Wilfried Zaha (25) kuchezea timu ya England dhidi ya Ivory Coast. (Mail)
Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham wanampango wa kurejea juhudi za kupata fedha zaidi kutoka kwa marupurupu wanaolipia nchi za nje kutangaza mechi za Premier League. (Mail)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment