May 1, 2018



Na George Mganga


Nyota wa Bongo Fleva nchini Ali Saleh Kiba 'Alikiba' amezindua rasmi bidhaa yake mpya ya kinywaji inayojulikana kwa jina la Alikiba Mofaya Energy Drink itakayoanza kusambaa mitaani hivi karibuni.

Kiba ameitambulisha bidhaa ya kinywaji hicho katika Ukumbi wa Serena Hotel wakati wa sherehe za harusi yake iliyofanyika juzi Jumapili.



Msanii huyo amekuwa mmiliki wa bidhaa hiyo itakayoanzaa kupatikana Afrika Mashariki na baadaye itasambazwa katika sehemu mbalimbali duniani.

Kiba ameeleza kuwa ameamua kuileta Mofaya Afrika Mashariki akishirikiana na Msanii mwenzake Bulive kutoka ukanda wa Afrika.

Bidhaa hii imekuwa ni moja kati ya zile alizotangaza kutambulisha huku zikitajwa zingine kuwa atazindua siku za usoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic