May 1, 2018



Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaendelea leo katika mchezo wa marudiano kati ya Real Madrid watakaokuwa nyumbani kuikaribisha Bayern Munich.

Madrid watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu wakiwa na faida na bao moja kufuatia ushindi wa 2-1 ugenini kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.

Mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 3 na dakika 45 kwa saa za Afrika mashariki utatoa mshindi atakayetangulia kwenye hatua ya fainali ya mashindano hayo.

Mshindi wa pili atasubiriwa kesho ambapo majogoo wa Anfield, Liverpool watakuwa wageni dhidi ya AS Roma huko Italy.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic