May 4, 2018Na George Mganga

Kocha mpya wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo katika benchi la ufundi itakapovaana na USM Alger kwenye mechi ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Mkongo huyo amejiunga na Yanga hivi karibuni kuchukua nafasi ya Kocha, George Lwandamina aliyetimkia kwao Zambia kuifundisha Zesco United.

Zahera atakuwa anaweka rekodi ya kuinoa Yanga kwenye mechi hiyo ya kimataifa baada ya kukosekana kwenye mechi ya ligi dhidi ya Simba, Jumapili ya wiki iliyopita.

Mchezo huo wa makundi utakuwa ni wa kwanza kwa Yanga kufuatia droo ya makundi kupangwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Ukiachana na USM Alger, timu zingine zilizopangwa na Yanga kwennye kundi D ni Rayon Sports ya Rwanda pamoja na Gor Mahia FC ya Kenya.

2 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV