May 4, 2018Msanii wa Bongofleva Alikiba a.ka.a King Kiba ametoa ahadi kwa mashabiki wake ikiwa ni pamoja na kutoa changamoto kwa mashabiki kuweza kufikisha idadi ya watazamaji milioni tatu kwenye wimbo wa msanii Ommy Dimpoz aliomshirikisha Seyi Shay kutoka Nigeria.

Alikiba ametoa ahadi hiyo kwa mashabiki zake ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu alipoachia wimbo wa ‘Seduce Me’ ulioweza kuvunja rekodi ya kutimiza ya video zote za wasanii nchini kwa kuangaliwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya saa 38.

“Hii nyimbo Ya Ommy Dimpoz ikifika milioni 3 Youtube Naliamsha dude (I PROMISE U)”- Alikiba.

Alikiba na Ommy Dimpoz ni wasanii ambao wote wapo chini ya uongozi wa Rockstar4000.

Kutoka Global Publishers

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV