May 15, 2018



Baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapiga debe wa Stand United kutoka mkoani Shinyanga, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amewabatiza jina jipya wapinzani wake.

Bwire ameamua kuwabatiza jina jipya Stand kufuatia kupoteza alama tatu muhimu jana kwa kuwaita kuwa ni wapiga POPO kutokana na aina ya upinzani waliouonesha.

Msemaji huyo ameamua kuwabatiza jina jipya Stand United huku akijigamba kuwa wao wapo kwa ajili ya kupapasa akieleza hawana utani hivi sasa.

Kikosi hicho cha Ruvu Shooting jana kimejiongeza pointi tatu muhimu kwa kufikisha 33 kwenye nafasi ya 7.

Stand wameendelea kusalia katika nafasi yao ya 9 wakiwa na pointi 32 huku wakiwa wamecheza michezo 27 msimu huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic